Jumamosi 23 Mei 2026 - 11:34
Khorramshahr yetu ya leo ni kuulinda Mlango wa Hormuz na kuvunja utukufu wa Marekani/ Adui anajitahidi kuigawanya jamii katika makundi mawili na kueneza mifarakano katika mikusanyiko

Hawza/Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qum alisisitiza kuwa: Imam mtukufu marehemu alisema: “Khorramshahr aliikomboa Mwenyezi Mungu.” Hii ni kanuni kwamba kila mahali tuliposimama kwa mapambano na uthabiti, Mwenyezi Mungu alitufungulia njia, leo pia Khorramshahr yetu ni kutoka katika mzingiro wa kiuchumi, kuulinda Mlango wa Hormuz na kuvunja utukufu wa kijeshi na kisiasa wa Marekani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari wa Shirika la Habari la Hawza,Ayatullah Sayyid Muhammad Saeedi, katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 1 Khordad 1405 (22 May 2026) zilizofanyika katika Muswala wa Quds mjini Qum Iran, kuhusu uchambuzi wa ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuhusu idadi ya watu na kuzaa watoto alisema: Idadi ya watu ni mfano wa nguvu ya taifa na kina cha kimkakati, kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi haioni idadi ya watu kama takwimu tu, bali anaiona kuwa ni mtaji wa kibinadamu na msingi mkuu wa nguvu ya taifa, Iran yenye nguvu inahitaji kizazi cha vijana, chenye hamasa na wasomi mahiri.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum alisisitiza: Bila nguvu ya vijana, mzunguko wa kisayansi, wa ulinzi na wa kiuchumi wa nchi utapungua kasi, hivyo, kuzaa watoto ni jihadi kwa ajili ya kuendelea kuwepo na kustawi kwa Iran.

Aliendelea kusema: Kuvuka shimo la kupungua kwa idadi ya watu ni jambo la dharura la haraka, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi alisisitiza kwamba; fursa yetu ya kuzuia muundo wa idadi ya watu wa Iran kuzeeka ni fupi sana, uchambuzi wa ujumbe wake unaonyesha kuwa tupo katika hatua nyeti ya kihistoria ya idadi ya watu, ikiwa leo hakutakuwa na mipango sahihi, katika miongo ijayo tutakabiliwa na mgogoro wa watu wa umri wa kati na wazee, jambo ambalo litaleta gharama kubwa za matibabu na kupungua kwa uwezo wa uzalishaji.

Mwakilishi wa Walii Faqihi mjini Qum aliongeza: Katika ujumbe wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kuna ufafanuzi madhubuti wa tauhidi, kwa kukosoa mitazamo ya kimada inayomwona mtoto kuwa gharama, alisisitiza ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu riziki: «نَحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَ إِیَّاکُمْ», Uchambuzi wa mtazamo huu unamaanisha kwamba; kumtegemea Mwenyezi Mungu kunapaswa kuchukua nafasi ya hofu ya umaskini ili kuondoa mafundo ya kifikra ya familia nyingi.

Akiashiria kwamba Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi aliyataka makundi mawili—maafisa na wasomi—kutekeleza wajibu wao, alibainisha: Maafisa wanapaswa kuondoa vikwazo vya maisha, makazi na ajira kwa vijana ili ndoa na kuzaa watoto viwe rahisi, pia wasomi na wahubiri wanapaswa kuondoa mafundo ya kitamaduni na ya kiakili ya watu, kwa sababu sehemu kubwa ya kupungua kwa idadi ya watu inatokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha na mashambulizi ya kitamaduni ya adui, jambo ambalo linapaswa kurekebishwa kupitia jihadi ya ufafanuzi.

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Idadi ya watu ni kipengele cha kujenga ustaarabu wa Kiislamu, kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi, ustaarabu mpya wa Kiislamu unahitaji safu pana ya wafuasi wa Ahlul-Bayt (as), kuongezeka kwa kizazi ni sawa na kuimarisha safu ya haki na kuandaa mazingira ya kudhihiri Imam Mahdi (ajf).

Alikumbusha kuwa: Suala la idadi ya watu ni wajibu na hitaji muhimu kwa mustakabali wa nchi, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi kwa mtazamo wa hekima anatahadharisha kwamba; haipaswi kuruhusiwa Iran kuwa nyumba ya wazee, kufufua idadi ya vijana ni jihadi ya kiuchumi, kitamaduni na kiulinzi, na ni sababu ya furaha kwa Mtume Mtukufu (saww) ambaye Siku ya Kiyama atajivunia wingi wa umma wake.

Adui anataka kueneza mifarakano katika jamii

Akiendelea na mazungumzo yake, huku akisema kwamba kuhifadhi umoja ni pigo kubwa zaidi kwa adui na kwamba kuheshimu hijabu ni alama ya utambulisho wa kimapinduzi wa jamii, aliongeza: Umoja ndio silaha yetu kubwa zaidi mbele ya safu ya ukafiri.

Adui ameshindwa katika medani ngumu za mapambano, na kwa sababu hiyo anataka kuigawanya jamii katika makundi mawili na kueneza mifarakano katika mikusanyiko, kwa hiyo tunapaswa kuwa waangalifu katika mazungumzo yetu na katika mitandao ya kijamii ili tofauti za mitazamo zisigeuke kuwa migawanyiko, siri ya ushindi wetu ni mshikamano.

Haya na nidhamu ya kijamii ni mstari wetu mwekundu

Khatibu wa Ijumaa wa Qum akiwaelekea wanawake alisema: Hijabu si kizuizi kwenu, bali ni ngome ya heshima, utukufu na usalama, stara yenu ni urithi wa Bibi Fatimah Ma’sumah (as), adui anajaribu kudhoofisha ghera ya kidini na maadili ya jamii, lakini wanawake wa kimapinduzi hawataruhusu namna yao ya mavazi itumike kuupinga mfumo.

Alisema kuwa: Wananchi wa kimapinduzi wanatarajia vyombo vya usalama na mahakama kwamba katika kulinda mipaka ya stara na usalama wa kisaikolojia wa jamii kusiwe na uzembe wowote, inapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa uthabiti dhidi ya kutovaa hijabu, uvunjaji wa maadili uliopangwa na pia jambo la kutembeza mbwa, haya na nidhamu ya kijamii ni mstari wetu mwekundu.

Imamu wa Ijumaa wa Qum, huku akiadhimisha Siku ya Khorramshahr (3 Khordad), alisema: Imam mtukufu marehemu alisema: “Khorramshahr aliikomboa Mwenyezi Mungu.” Hii ni kanuni kwamba kila mahali tulipofanya mapambano ya uthabiti, Mwenyezi Mungu alitufungulia njia, leo pia Khorramshahr yetu ni kutoka katika mzingiro wa kiuchumi, kulinda Mlango wa Hormuz na kuvunja utukufu wa kijeshi na kisiasa wa Marekani.

Msimamizi wa Haram Takatifu ya Bibi Fatimah Ma’sumah (as) aliendelea kusema: Ikiwa leo Marekani ipo katika hali ya udhaifu na fedheha, na masharti yetu yanajadiliwa kutoka katika nafasi ya nguvu, ni kwa sababu watu wetu wamefanya mantiki ya Khorramshahr, yaani mantiki ya mapambano ya uthabiti, kuwa kaulimbiu yao.

Alisema: Leo ni wazi kwa kila mtu kwamba sera za kiburi cha dunia zimefeli mbele ya Iran, wale waliokuwa na ndoto ya kuisambaratisha Iran leo wanakabiliwa na migogoro ya ndani na kutengwa kimataifa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa uongozi wa hekima wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi na kwa kutegemea kina chake cha kimkakati katika eneo, ina nguvu zaidi kuliko wakati wowote ule, sisi hatuzungumzi kutoka katika nafasi ya dharura, bali kutoka katika nafasi ya nguvu yenye kudai haki.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum alisisitiza: Adui ajue kwamba zama za kupiga na kukimbia na kulazimisha mikataba ya upande mmoja zimekwisha, kila mtu ajue kwamba heshima yetu ya leo si sadaka kutoka kwa mtu yeyote, bali ni matokeo ya dhulma, nguvu na damu safi ya Imam shahidi wa umma, ushindi wetu wa leo unatokana na uongozi wa Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, heshima na nguvu yetu ya leo vinatokana na damu ya mashahidi, mapambano ya uthabiti na uwepo wa watu mashujaa na wafuasi wa Wilaya.

Dhamira haiwezi kuangamizwa kwa mabomu

Akiashiria Siku ya Ustahimilivu na Uthabiti alisema: Dezful ni mfano wa mapambano na uthabiti, Dezful ilithibitisha kwamba mashambulizi ya mabomu na makombora yanaweza kubomoa nyumba, lakini hayawezi kuvunja dhamira, Dezful ni medali ya fahari ya uthabiti kifuani mwa Iran na ni mfano wa kuigwa katika kusimama dhidi ya mashinikizo makali ya leo.

Msimamizi wa Haram Takatifu ya Bibi Ma’sumah (as) aliongeza: Mashahidi wa huduma walithibitisha kwamba mtu anaweza kuwa mwanamapambano wa medani, mwanadiplomasia stadi, Imamu wa Ijumaa bora na gavana mwenye sifa kwa wakati mmoja, inawezekana badala ya kutazama mikononi mwa “kiongozi wa kijiji”, kutegemea uwezo wa ndani na mahusiano ya busara ili kumweka adui katika hali ngumu, nguvu na heshima tulizonazo leo katika medani, mitaani na nje ya nchi pamoja na eneo zimetokana na upangaji huo sahihi wa njia na juhudi zisizochoka.

Akiashiria Siku ya Tija na Uboreshaji wa Matumizi alisema: Taqwa katika uwanja wa uchumi ina maana ya kutumia rasilimali kwa ufanisi, israfu na ubadhirifu ni vizuizi vya maendeleo ya nchi, usimamizi sahihi wa rasilimali na nishati si ushauri wa kimaadili tu, bali ni jihadi ya kitaifa kwa ajili ya kufanya vikwazo visiweze kuathiri.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha